Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Maqsood Ali Domki, mwanachama mwandamizi wa Majlisi ya Muungano wa Waislamu Pakistan, katika mkutano na waandishi wa habari katika jimbo la Sindh aliitaja hali ya sasa ya Palestina na wajibu wa umma wa Kiislamu, alisisitiza kuendelezwa kwa misingi ya asili ya waasisi wa Pakistan na kujitolea kwa dhati kwa taifa lililoteseka la Palestina.
Aliongeza kuwa: taifa la Pakistan lenye watu wapatao milioni 250 bado limebaki na imani thabiti na dira ile ile ambayo waasisi wa nchi waliibeba, kiongozi muadhamu Muhammad Ali Jinnah na Allama Iqbal—ndiyo msingi wa Pakistan. Taifa letu bado linashikilia kanuni kwamba Palestina ni taifa la Wapalestina na hakuna mamlaka inayostahili kuingilia kati katika kuamua hatima yao.
Akikosoa vikali sera za Marekani na utawala wa Kizayuni, alidai: mustakabali wa Palestina ni jukumu la Wapalestina pekee. Marekani na Israel zina haki gani za kuamua kwa niaba ya Wapalestina? Wale ambao ni sababu ya ukoloni na kifo hawawezi kuwa mahakimu wa haki.
Mwanazuoni huyo alibainisha juu ya mauaji ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni katika ukanda wa Ghaza akasema: kusitishwa kwa vita sio kuwasamehe wahalifu. Utawala wa Kizayuni, kwa msaada wa nguvu za kibandia, umeuwa zaidi ya watu 70,000 wasio na hatia huko Ghaza. Marekani na Israel zinapaswa kujibu kutokana na uhalifu huu wa kimbari, na wahusika wa uhalifu huu, wakiwemo Donald Trump, wanapaswa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
Hujjatul-Islam Domki alibainisha pia kuwa: uvamizi wa ardhi ya Palestina na Israel ni kitendo haramu, kinyume cha maadili na kinyume cha kanuni za kibinadamu, na hauwezi kuhalalishwa kamwe. Umma wa Kiislamu una wajibu wa kusimama dhidi ya dhuluma hii ya kihistoria na kuendelea kulisaidia taifa la Wapalestina hadi kushinda kabisa.
Maoni yako